1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Afrika Kusini yaadhimisha miaka 30 ya demokrasia

Tatu Karema
27 Aprili 2024

Afrika Kusini leo inaadhimisha miaka 30 ya demokrasia ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kufanyika uchaguzi wenye ushindani mkubwa katika miongo kadhaa

https://p.dw.com/p/4fG2d
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akiwasili katika mkutano wa pili wa Urusi na Afrika kusini nchini Urusi mnamo Julai 28, 2023
Rais wa Afrika Kusini Cyril RamaphosaPicha: Stanislav Krasilnikov/TASS/dpa/picture alliance

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amepongeza mafanikio ya nchi hiyo chini ya uongozi wa chama chake cha African National Congress (ANC).

Wakati wa hotuba aliyoitoa katika Majengo ya Muungano mjini Pretoria ambayo ndio makao makuu ya serikali, Ramaposa amesema kuwa kwasasa Afrika Kusini ipo mahali pazuri zaidi kuliko ilivyokuwa miaka 30 iliyopita.

Ramaphosa aisifia miaka 30 ya utawala wa ANC

Rais huyo pia ameongeza kuwa wamefuatilia mageuzi ya ardhi, na kutoa mamilioni ya hekta za ardhi kwa wale waliopokonywa ardhi zao kwa nguvu, kujenga nyumba, zahanati, hospitali, barabara na madaraja, mabwawa, na miundombinu kadhaa.

Soma pia:ANC yaadhimisha miaka 112 ya kuasisiwa kwake Afrika Kusini

Ramaphosa mwenye umri wa miaka 71 pia ametumia fursa hiyo kuelezea mafanikio na maboresho yaliyofanywa na chama cha ANC, ambacho kinakabiliwa na ushindani mkali katika uchaguzi ujao huku kikiwa katika hatari ya kupoteza kwa mara ya kwanza wingi wa wabunge.