1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manusura wa jengo lililoanguka Afrika Kusini bado watafutwa

10 Mei 2024

Matumaini yanazidi kufifia ya kuwapata wafanyakazi 44 wa ujenzi waliokwama kwa siku kadhaa katika kifusi cha jengo lililoporomoka nchini Afrika Kuisni.

https://p.dw.com/p/4fhKl
Jengo liliporomoka mjini George
Waokoaji wanakabiliwa na changamoto ya kuondoa tani za saruji kwa kutumia mashine nzito kuwatafuta manusuraPicha: Shafiek Tassiem/REUTERS

Matumaini yanazidi kufifia ya kuwapata wafanyakazi 44 wa ujenzi waliokwama kwa siku kadhaa katika kifusi cha jengo lililoporomoka nchini Afrika Kuisni. Mamlaka zinasema waokoaji wanakabiliwa na changamoto ya kuondoa tani za saruji kwa kutumia mashine nzito ili kuona kama kuna watu bado wako hai.

Soma pia: Manusura zaidi wapatikana mkasa wa kuanguka jengo Cape Town

Idadi ya watu waliokufa katika ajali hiyo ilipanda na kufikia watu 9, baada ya mfanyakazi mmoja aliyekuwa katika hali mbaya hospitalini kufariki. Kati ya wafanyakazi 28 waliookolewa, 21 wako katika hali mbaya kufuatia kuporomoka kwa jengo la ghorofa 5 ambalo lilikuwa katika ujenzi.

Wakati wasiwasi ukiongezeka kuhusu idadi ya vifo kupindukia 50, mamlaka katika mji wa George huko mashariki mwa pwani ya Afrika Kusini, zinasema vifaa vizito vimewasili na kwamba timu ya uokoaji inaendelea kuondoa vifusi na mabaki ya saruji kuwatafuta manusura.