1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Matumaini yanafifia waliokwama kwenye jengo Afrika Kusini

Sudi Mnette
9 Mei 2024

Ndugu wa wafanyakazi 44 wa ujenzi waliokwama katika jengo lililoporomoka la mji wa George Afrika Kusini wameingia siku ya nne ya kusubiri nusura ya jamaa zao wakati juhudi za kutafuta manusura wote zikiendelea.

https://p.dw.com/p/4fg9Z
Wafanyakazi wa uokoaji wakiendelea na shughuli za kuwatafuta waathirika katika jengo lililoporomoka Afrika Kusini.
Wafanyakazi wa uokoaji wakiendelea na shughuli za kuwatafuta waathirika katika jengo lililoporomoka Afrika Kusini.Picha: Esa Alexander/REUTERS

Kwa mujibu wa taarifa manispaa ya George kati ya watu 81 ambao walikuwa wakati jengo la ghorofa tano likiporomoka Jumatatu, wanane wamethibitishwa kufa na 29 wamekutwa hai, 16 kati yao wakiwa katika hali mbaya.

Utambulisho wa watu wanaohisiwa kuwa katika jengo hilo bado haujawekwa wazi, lakini orodha ya majina ilikuwa ikisamabazwa kati ya vikundi vya jamaa ambao wamekusanyika kwenye eneo la tukio tangu Jumatatu.

Soma pia:Manusuza zaidi wapatikana mkasa wa kuanguka jengo Cape Town

Hakuna taarifa mpya kutoka kwa kitengo cha cha uokozi katika eneo hilo na sababu za kuporomoka bado hazijawekwa wazi katika tukio hilo ambapo pia Rais Cyril Ramaphosa ametaka uchunguzi ufanywe.