1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Rais wa Korea Kusini akirii 'mapungufu' katika hotuba yake

Sudi Mnette
9 Mei 2024

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol amefanya mkutano na waandishi wa habari wa nadra, akikiri "mapungufu" baada ya chama chake kushindwa katika uchaguzi wa hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/4ffQA
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk YeolPicha: KIM MIN-HEE/Reuters

Aidha kiongozi huyo aliweka wazi sera zake katika suala la kuzorota kwa uzazi nchini humo na vita vya Urusi nchini Ukraine.

Kuhusu Ukraine, Yoon ameonesha dhamira kuwa na uhusiano thabiti na Kyiv huku akidumisha uhusiano mzuri na Urusi na kuwaambia waandishi wa habari kuwa ni "msimamo wake thabiti" kutopeleka silaha hatari kwa nchi zilizovitani.

Na katika suala la tatizo la kiwango duni cha uzazi cha Korea Kusini, mojawapo ya nchi zilizo kiwango cha chini zaidi duniani, alifichua mipango ya kuunda wizara ya kushughulikia suala hilo, ambalo alilitaja kuwa "dharura ya kitaifa".

Soma pia:Korea Kaskazini yaionya Marekani kuacha kuchanganya siasa na haki za binaadamu

Mkutano huo wa waandishi wa habari ulikuwa wa kwanza kwa rais huyo katika takriban miaka miwili, na unakuja baada ya chama chake kukumbwa na misukosuko katika uchaguzi wa wabunge mwezi uliopita.