1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi, Iran na China kufanya mazezi ya pamoja ya kijeshi

Sudi Mnette
12 Machi 2024

Meli ya kusafirisha makombora ya Urusi, Varyag imewasili katika bandari ya Iran ya Chabahar, tayari kwa kushiriki mazoezi ya pamoja ya kijeshi yatakayojumuisha mataifa ya Iran na Uchina katika Ghuba ya Oman.

https://p.dw.com/p/4dPRo
Meli ya kubeba makombora ya Kichina
Meli ya kubeba ndege ya China ambayo huenda ikaongeza wasiwasi katika mizozo ya maeneo la bahari.Picha: AP

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Interfax helikopta tatu za Irani zitaungana na meli nyingine kwa mazoezi hayo yaliopewa jina la "Ukanda wa Usalama wa Baharini  2024" ambayo yanalenga kuweka usalama kwa shughuli za kiuchumi kwenye usafiri wa bahari.

Ujia wa bahari wa Hormuz unaounganisha Ghuba ya Oman na Ghuba ya Uajemi ni njia kuu ya meli katika biashara ya kimataifa ya usafirishaji wa mafuta.

Shirika la Habari la Iran Tasnim limeripoti kuwamalengo ya zoezi hilo ni kupambana na uharamia na ugaidi wa baharini katika kanda, huduma za kiutu, ubadilishanaji wa taarifa juu ya uokoaji baharini na uzoefu wa kiutendaji na kimbinu.