1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Iran na China zatia saini makubaliano ya ushirikiano

Tatu Karema
27 Aprili 2024

Mawaziri wa ulinzi wa China na Iran wametia saini makubaliano ya ushirikiano pembezoni mwa mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Usalama ya Shanghai (SCO) unaofanyika nchini Kazakhstan

https://p.dw.com/p/4fG4v
Mkuu wa jeshi la wanamaji la China Dong Jun (kushoto) na Brigadia jenerali wa Iran Mohammed-Reza Astiani (kulia) wafanya mkutano nchini Kazakhstan Aprili 26, 2024
Mkuu wa jeshi la wanamaji la China Dong Jun (kushoto) na Brigadia jenerali wa Iran Mohammed-Reza Astiani (kulia)Picha: IRNA

Brigadia jenarali wa Iran Mohammed-Reza Astiani, amesema kuimarishwa kwa ushirikiano na ukaribu wa pande zote kunahitajika kutatua changamoto za kiusalama za kikanda na kimataifa.

Astiani ameyasema hayo baada ya mazungumzo na mkuu wa jeshi la wanamaji la ChinaDong Jun katika mji mkuu wa Kazakhstan, Astana.

Iran imetengwa kimataifa

Iran imetengwa kimataifa kwa sababu ya mpango wake wa nyuklia na uungaji wake mkono kwa makundi ya wapiganaji katika eneo la Mashariki ya Kati. Kukabiliana na hatua hiyo, serikali mjini Tehran imeimarisha uhusiano wake na Urusi na China.

Na katika harakati za kutafuta washirika wapya, Iran ilijiunga na Jumuiya ya SCO mwezi Julai mwaka jana.